Yohana 17:22 — "Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja."
Karibu ushiriki nasi katika ibada zetu za wiki na Jumapili kupata chakula cha kiroho na ushirika.
Venue: Main Sanctuary Church
Muda: 07:30 AM - 12:00 PM
Kiongozi: Mch Motomkali
Venue: Fellowship Hall
Muda: Jumamosi, 05:00 PM - 06:30 PM
Kiongozi: Judith Masawe
Venue: Kids Room / Youth Center
Muda: Jumapili, 08:00 AM (Watoto) / Jumamosi, 03:00 PM (Vijana)
Kiongozi: Blandina Kitundu / Sonia
Tazama ibada zetu moja kwa moja kupitia YouTube Live na Facebook Live. Kama hatuko hewani kwa sasa, kihesabu (countdown) hapa chini kinaonyesha muda uliobaki hadi ibada inayofuata ya Jumapili asubuhi.
"Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu, asema Bwana. Kama mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu."Isaya 55:8-9
Wakati mwingine tunapitia changamoto na kupanga mipango yetu tukiamini ndiyo njia bora zaidi. Lakini Mungu ana picha kubwa zaidi ya maisha yetu. Kujisalimisha kwenye njia zake hutuletea amani isiyo na mwisho.
"Baba Mtakatifu, ninaomba unipe moyo wa kukutumaini hata pale ambapo njia zako sizielewi. Ninaachilia mipango yangu mikononi mwako. Amina."
Jiunge na maelfu ya waumini wanaosoma Biblia kila siku kwa kutumia ratiba yetu ya kusoma kwa mwaka mzima.
Kila idara ni fursa ya kukua kiroho na kutumika kwa vipawa ulivyopewa na Mungu.
Kusikia jinsi Mungu anavyobadilisha maisha ya waumini katika uponyaji, wokovu, na ukombozi huleta imani.
"Nilisumbuliwa na tatizo la mgongo kwa zaidi ya miaka mitatu, nilishindwa hata kuinama. Baada ya kuombewa katika ibada ya Ijumaa na Mch Motomkali, niliponywa kabisa na sasa nafanya kazi bila maumivu!"
"Familia yetu ilikuwa kwenye migogoro mizito na tishio la talaka. Tulipokuja kwenye ibada ya maombezi, Mungu alirejesha amani na upendo."
"Nilikuwa nimezama kwenye ulevi na kukata tamaa ya maisha. Nilipokaribishwa kanisani nilimkabidhi Yesu maisha yangu. Nimekuwa kiumbe kipya."
Sadaka na michango yako inatusaidia kueneza Injili ya wokovu na kuboresha miundombinu ya kanisa letu. Unaweza kutoa Sadaka ya Kawaida, Usemasi, au Sadaka ya Ujenzi salama kabisa.